EAC Logo

 
 
Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zanzibar, Mhe. Hamis Said akitoa hotuba yake.

Jumuiya ya Afrika Mashariki yaanza maadhimisho ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani

Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha, Tanzania, 6th July 2022: Mamia ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutoka bara zima la Afrika wamekusanyika Zanzibar, katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani, iliyopangwa kufanyika tarehe 7 Julai 2022.  Hafla ya maadhimisho haya hii imewaleta pamoja wahimizaji wa utumizi wa lugha ya Kiswahili kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wakiwemo walimu na wanafunzi na wanahabari. Maadhimisho yamendaliwa na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (East Africa Kiswahili Commission) , taasisi iliyo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community). 

Maadhimisho ya lugha ya kiswahili yenye Kauli Mbiu: Kiswahili kwa Amani, Ustawi na Utangamano wa Kikanda yanatokana na uamuzi wa Kikao cha 41 cha Shirika la Umoja wa Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika tarehe 5 Novemba 2021. Uamuzi huo umeipa lugha ya Kiswahili kipaumbele kwa kuridhia maombi ya kuwa na Siku ya Kiswahili Duniani. Kutokana na uamuzi huo Siku ya Kiswahili Duniani itaadhimisha 7 Julai kila mwaka. 

Umuhimu wa Zanzibar kupewa nafasi kwanza ya kuandaa maadhimisho ya Kiswahili ni kwa kuzingatia kuwa Zanzibar ndio makao makuu Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA) tahasisi iliyo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendeleza na kuratibu maendeleo ya Kiswahili i.e yenye makao yake makuu Zanzibar.  

Jumuiya ya Afrika Mashariki inatoa shukrani zake kwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Zanzaibar kwa kutupatia makao makuu ya Kakama huko Zanzibar. 

Baadhi ya wadau wa Kiswahili walioudhuria Maadhimisho Lugha ya Kiswahili Zanzibar

Akizungumza kwenye kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zanzibar, Mhe Hamis Said kwa niaba ya Waziri Tabla Manlid Mwita alisema, "Kiswahili kinatakiwa kitumike kama ni bidhaa inayouzwa na kupata tija. Kwa sasa, kuna haja kubwa ya kuwekeza kuwasomesha wataalamu wetu wa lugha kuwa na stadi na ukalimani, kutafrisi na kuandaa machapisho mbali mbali kwa Kiswahili. "

Mhe. Naibu Katibu Mkuu alisema kuna haja kubwa ya kuwekeza kwa kiasi kikubwa kuwasomesha wataalamu wetu wa lugha kuwa na ustadi na uwezo unaotaliwa katika kutoa huduma ya kufundisha, ukalimani kutafsiri na kuandaa machapisho mbali mbali kwa kiswahili. 

Mhe. Said ametoa wito kwa wasomi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kutilia mkazo sana uwekezaji wa kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili na vile vile kufanya tafiti mbali mbali za lugha. 

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote akiongea na wadau wa kiswahili wakati wa ufuguzi wa maadhimisho ya lugha ya kiswahili.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote alibainisha kuwa ni jukumu la vyuo vikuu vyetu vya Afrika Mashariki kutilia mkazo sana uwekezaji wa kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na vile vile kufanya tafiti mbali mbali za lugha.

"Uteuzi wa Kiswahili kama lugha ya matumizi mapana na pia lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umeweka mazingira mwafaka wa kuendeleza matumizi ya Kiswahili kikanda na kimataifa. Kiswahili sasa kina upeo mkubwa na hadhi yake inazidi kuimarika, " alisema Mhandisi Mlote.

Maadhimisho ya kiswahili yatafika killele chake kesho tarehe 7/07/2022 huku rais wa Zanzibar Mh. Hussein Mwinyi akitegemewa kuwa mgeni rasmi. 

Tags: #KiswahiliDay2022


East African Community
EAC Close
Afrika Mashariki Road
P.O. Box 1096
Arusha
United Republic of Tanzania

Tel: +255 (0)27 216 2100
Fax: +255 (0)27 216 2190
Email: eac@eachq.org  |  sgoffice@eachq.org